JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb.Na.JA.9/259/01/C/5 16 Oktoba, 2025
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya na MDAs & LGAs
anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza
nafasi 17,710 kama ilivyoainishwa katika tangazo hili;
3.1 MAJUKUMU YA KAZI
i.Kuandika na kutunza “register” zinazohusu shughuli za uhasibu;
ii.Kutunza kumbukumbu za hesabu;
iii.Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki; na
iv.Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Cheti cha Astashahada ya Uhasibu kutoka Chuo kinachotambulika na
Serikali au Cheti cha ATEC I kinachotolewa na NBAA au sifa nyingine zinazolingana na
hizo zinazotambulika na NBAA.
3.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGS. B
MASHARTI YA JUMLA
1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa
kwa wale tu walioko kazini serikalini.
2. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa
kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya
taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
3. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
4. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili.
5. Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma, WASIOMBE na
wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba
CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
6. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti
vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha
Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:-
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
Computer Certificate
Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
7. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato
cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
8. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
9. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
10. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
11. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 29 Oktoba, 2025.
12. Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyetivya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.
13. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal)
kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye
tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment
Portal’).
14. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.
Limetolewa na:
KATIBU
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
APPLY NOW
JOIN US TODAY
WHATSAPP GROUP 1
WHATSAPP GROUP 2
WHATSAPP GROUP 3
TELEGRAM
Discover more from Mwanampotevu Digital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.