Posted in

AFISA TAWALA DARAJA LA II (ADMINISTRATIVE OFFICER GRADE II) – Nafasi 32 – MDAs & LGAs – UTUMISHI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb.Na.JA.9/259/01/C/5                                                                               16 Oktoba, 2025

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya na MDAs & LGAs
anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza
nafasi 17,710 kama ilivyoainishwa katika tangazo hili;

4.1 MAJUKUMU YA KAZI
i.Kutoa mapendekezo kuhusu utekelezaji wa Sheria, Sera, Kanuni na Taratibu
mbalimbali zinazotolewa na Serikali;
ii. Kutoa mapendekezo kuhusu kazi za utawala na uendeshaji katika Ofisi za Serikali;
iii. Kushughulikia masuala ya itifaki mahali pa kazi;
iv. Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu ya Taasisi;
v. Kupokea na kusajili malalamiko mbalimbali yanayowasilishwa;
vi. Kusimamia miundombinu ya Ofisi na Majengo; vii. Kushiriki katika maandalizi ya
Vikao vya Baraza la Wafanyakazi;

viii. Kushughulikia masula ya anuai za Jamii;
ix. Kuratibu shughuli za Maafa; na x. Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na kada yake
kama zitakavyoelekezwa na Msimamizi wa kazi

4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada katika mojawapo ya fani zifuatazo; Public Administration,
Political Science and Public Administration, Business Administration au Commerce
iliyojiimarisha katika (Human Resources Management), Leadership and Governance,
Public Administration and Management, Local Government and Management, Human
Resource Planning and Management, Human Resources Management, Human
Resources Planning, Labour Relations and Public Management, Industrial Relations, au
fani nyingine zinazoendana na hizo kutoka katika Taasisi au Vyuo vinavyotambulika na
Serikali.
4.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGS.E

MASHARTI YA JUMLA
1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa
kwa wale tu walioko kazini serikalini.
2. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutumia maombi na wanapaswa
kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya
taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
3. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.

4. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili.
5. Waombaji kazi ambao ni waajiriwa katika Utumishi wa Umma, WASIOMBE na
wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyopo katika waraka namba
CAC45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
6. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti
vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha
Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika:-
Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
Computer Certificate

Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
7. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato
cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
8. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
9. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
10. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
11. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 29 Oktoba, 2025.
12. Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyetivya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
DODOMA.
13. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal)
kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana kwenye
tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment
Portal’).
14. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.

Limetolewa na:
KATIBU
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

APPLY NOW 

JOIN US TODAY

WHATSAPP GROUP 1

WHATSAPP GROUP 2

WHATSAPP GROUP 3

LINKEDIN

TELEGRAM


Discover more from Mwanampotevu Digital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *