WALIOITWA Kwenye Usaili Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 2025

WALIOITWA Kwenye Usaili Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 2025
WALIOITWA Kwenye Usaili Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 2025, Kuitwa Kwenye Usaili Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Machi 31, 2025.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anapenda kuwatangazia kuwa vijana waliomba ajira ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia mfumo wa ajira ZIMAMOTO RECRUITMENT (ajira.zimamoto.go.tz), Usaili utafanyika kuanzia tarehe 05 Aprili, 2025 hadi tarehe 17 Aprili, 2025 kuanzia saa 1:00 Asubuhi kwa kila kundi.
Waombaji waliomba ajira kwa elimu ya kidato cha nne usaili wao utafanyika kuanzia tarehe 05 hadi 09 Aprili, 2025 saa 1:00 Asubuhi kwenye mikoa walioichagua wakati wa kutuma maombi.
Waombaji wenye elimu ya Shahada na taaluma mbalimbali usaili wao utafanyika katika Ukumbi wa Andengenye Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Dodoma kuanzia tarehe 14 Aprili hadi 17 Aprili, 2025, saa 1:00 Asubuhi kwa kila kundi.
Zingatia yafuatayo:
- Kila mmoja anatakiwa kufika kwenye usaili siku na tarehe aliyopangiwa na si vinginevyo.
- Kuwa nadhifu na kuvaa mavazi ya staha.
- Kufika na vyeti vyote halisi vilivyotumika kwenye maombi ya ajira kama vile cheti cheti cha Kidato cha nne, Kidato cha sita, Cheti cha taaluma, cheti cha kuzaliwa, pamoja na Kitambulisho cha Taifa au Namba ya kitambulisho cha Taifa (NIDA)
- Kwa walioomba nafasi ya Udereva pamoja na maelekezo hayo wanatakiwa kuja na leseni halisi ya udereva Daraja E.
- Gharama za usafiri, chakula na malazi ni juu ya msahiliwa mwenyewe kwa muda wote utaotumika kwa ajili ya usaili.
- Vijana watako fanya usaili Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wazingatie tarehe zao za usaili, kijana atayekuja tarehe ambayo hajapangiwa hatapokelewa.
Orodha ya Vijana waliochaguliwa kufanya usaili pamoja na makundi hayo imeambatanishwa kwenye PDF hapa chini;