Tangu kuanza kwa mwaka huu tumeona makampuni mengi ya simu ya Kichuana vikali huyu akija na simu yenye processor yenge uwezo zaidi mwengine anakuja na simu yenye kamera kali zaidi na ushindani huu umekuwa mkubwa kufikia kampuni za baba mmoja Infinix na TECNO kuingia kwenye ushindani mkubwa.

Alianza TECNO kuja na Camon 17 pro simu ambayo sifa yake kuu ni selfie kamera ya MP48 Infinix akamjibu kikubwa kwamba simu ni ofisi akaja na Infinx NOTE 10 pro ambayo sifa yake kuu ni MediaTek Helio G95.

Kamera

Haijatosha simu ya Infinix NOTE 10 pro pamoja ya kuwa na kamera kuu MP64 sawa tu na Camon 17 pro lakini kamera ya Infinix NOTE 10 pro inauwezo wa kuscan document za kiofisi na nyenginezo.

 (Rom Na Ram)

Kwa upande wa uhifadhi wa ndani au ROM, Infinix Note 10 Pro inamzidi TECNO Camon 17 pro japo ya kuwa zote zina ROM ya GB 128 kwa 256 lakini, Infinix Note 10 Pro ina uwezo wa kuchukua memory card ya Hadi TB 2 tofauti na TECNO Camon 17 pro ambayo inaweza kuchukua Memory ya hadi TB 1 na kwa upande wa RAM simu hizi zinalingana zote zina GB 8. 

Battery

Kwa upande wa battery simu ya Infinix Note 10 Pro ni bora zaidi japo simu zote mbili zina mAh 5000 lakini Infinix NOTE 10 pro ina 33wh ambayo inasaidia simu kujaa chaji kwa haraka zaidi ukilinganisha na TECNO Camon 17 pro yenye 25Wh. Muda ambao utatumia kujaza chaji Infinix NOTE 10 pro ni mdogo kuliko muda utakaotumia kujaza chaji simu ya TECNO Camon 17pro. Kwa mtu mwenye matumizi mengi ni vyema kutumia Infinix NOTE 10 pro.

Kioo

Tukija kwenye upande wa kioo, Infinix Note 10 Pro pia inaongoza kwenye kipengele hichi kwa kuwa na kioo kikubwa zaidi, Infinix Note 10 Pro inakuja na kioo cha inch 6.95, tofauti na TECNO Camon 17 pro yenyewe inakuja na inch 6.8 ambapo kwenye swala zima la kuangalia movie au mpira na kucheza games utafurahia zaidi kupitia Infinx NOTE 10 pro.

Muundo

Tukianza na muundo simu ya Infinix Note 10 Pro ni simu bora kwenye kipengele hichi, hii inatokana na simu hii kuwa na muundo mkubwa kuliko TECNO Camon 17 pro. Infinix Note 10 Pro inakuja na urefu (height) inch 6.80, upana (width) inch 3.08, na kina (depth) inch 0.31. TECNO Camon 17 pro yenyewe inakuja na urefu inch 6.65, upana ni inch 3.03, na kina inch 0.35. hapa Infinix NOTE 10 pro ni kubwa zaidi.

Upatikanaji

Simu zote hizi zinapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania zikiwa na ofa ya GB 78 kwa mwaka mzima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *